Dhibiti Mlipuko: COVID-19 Tanzania

Dhibiti Mlipuko: COVID-19 Tanzania

Mlipuko wa Corona unatishia usalama wa maisha ya Wataanzania walio wengi. Bila tahadhari ya haraka na ya kutosha, wengi wanaweza kupata maambukizi, na hata kupoteza maisha yao. Tunahitaji kushirikiana kwa haraka, pamoja na ndugu zetu nyumbani, kupigana  na vita hii.

Kama mtanzania uishio nje ya Tanzania (Diaspora), tunaomba mchango wako wa kifedha kufanikisha jitihada za kudhibiti mlipuko wa COVID-19 nyumbani. Kampeni hii ya “Dhibiti Mlipuko: COVID-19 Tanzania” ni kampeni inayohusisha ushirikiano wa taasisi na jumuiya za watanzania kwenye majimbo mbalimbali ya marekani.

Njia za Utumaji wa Michango: Pamoja na GoFundMe, unaweza kuwakilisha mchango wako kupitia CashApp ($TZDiaspora au namba ya simu 612 229 2919).

Tarehe ya mwisho ya kuwakilisha michango ni 31 Mei, 2020

Ugawaji wa Mchango:  Tunazingatia na kuweka kipaumbele kuimarisha usalama wa watoa huduma, ikiwa ni pamoja na wahudumu wa afya, wafanyakazi wa huduma za dharura, na hata wanaohakikisha usalama wa raia. Ijulikane kwamba mlipuko unaenda kwa kasi, na mahitaji yanabadilika, tunaendelea kuwa karibu na wadau husika nyumbani na kupata taarifa za juhudi zinazoendelea ili kupata tathmini ya mahitaji yenye vipaumbele. Hii itatupa mwongozo kwenye maamuzi ya mwisho ya ugawaji wa misaada muda ukifika.

Tafadhali zingatia yafuatayo:
1.  Kama unatumia CashApp au Zelle, tafadhali tunaomba bofya hapa (TAARIFA YA MCHANGIAJI  ) ututumie jina lako, anuani ya barua pepe na namba ya simu, ili tukutumie barua kwa ajili ya punguzo la kodi (tax return).
2.  Kama unatumia Zelle kutuma mchango, unahitaji  kufuata maelezo hapa -ZELLE  . Kama unatuma mchango wako kupitia benki, tafadhali pata taarifa za benki kupitia hapa – BANK WIRE INFORMATION .
3.  Barua zitatolewa kwa wale tu waliochangia kiwango cha kuanzia US$250, kufuatana na kanuni za US Internal Revenue Service.
4.  Kampeni hii inaratibiwa na kamati ya watanzania wachache waliojitolea, ikishauriwa na viongozi wa jumuiya na taasisi. Uhasibu wa michango unasisimamiwa na taasisi ya DICOTA .
5.  Usimamizi wa utoaji wa msaada kutoka kwenye michango utafanyika kwa ushirikiano na viongozi wa jumuiya, na ripoti ya uhasibu itatolewa kwa wachangiaji baada ya zoezi zima kuisha.

Aidha, tunakusihi ujikinge na uwakinge wenzako: Kaa nyumbani, Osha mikono, Tumia barakoa, na Epuka mikusanyiko.
Umoja wetu, ndio nguvu yetu.

Asanteni!

N.B: Wasiliana nasi kwa barua pepe -- dhibiticovidtz@gmail.com

Kwa Maelezo Zaidi: Pitia Maswali ya Mara kwa Mara 

***********************************************************************************************************************************************************
The coronavirus pandemic is threatening the safety and lives of many Tanzanians. Without emergency prevention efforts, many will succumb to infection and even lose their lives. We need prompt collaborative action, together with our people at home, to fight this war.

As a Tanzanian living abroad (diaspora), we ask for your financial donation to contribute towards response efforts to curb the COVID-19 pandemic at home. This campaign is a partnership of organizations and associations of Tanzanians living in different states in America.

Ways to send your donation:
In addition to GoFundMe, you can also contribute via CashApp ($TZDiaspora or phone number 612 229 2919)

The last day to submit your donation is 15th May 2020

Fund Disbursement: We are prioritizing efforts to ensure the safety of frontline workers, including healthcare workers, emergency services, and even those ensuring the safety of civilians. Since the pandemic and response efforts are rapidly evolving, we are liaising closely with key stakeholders at home to get information on ongoing efforts to assess priority needs. This will guide final decision-making on fund disbursement in the near future.

Please note the following:
1.  If you are using CashApp or Zelle, please click here (DONOR INFORMATION )to send your name, email address and phone number so we can send you an acknowledgment letter for your tax returns. 
2.  If you are using Zelle to donate, you need to follow the instructions available here - ZELLE. If you are sending your donation via bank wire, please see bank information here – BANK WIRE INFORMATION
3.  Acknowledgment letters will be sent via email to only those who donate an amount above $250, as per guidelines from the US Internal Revenue Service.
4.  The campaign is coordinated by a small committee of Tanzanian volunteers, with guidance and advice from leaders of different Tanzanian diaspora associations from different states and organizations. DICOTA is providing fiduciary support to this fundraising effort.
5.  Governance of fund disbursement from these donations will be done in collaboration with the leaders of different Tanzanian diaspora associations from different states and organizations, and a financial report will be provided at the end after this effort has been completed, and funds disbursed.

In addition, we ask you to protect yourself and others from infection. Stay at home, Wash your hands, Use a mask, and Avoid gatherings.

Our unity is our strength.

Thank You!

P.S: Please contact us via email at dhibiticovidtz@gmail.com 

For more information: Visit our Frequently Asked Questions

Donations

 • Modupeola Akinola 
  • $200 (Offline)
  • 2 d
 • Hajji Khatib 
  • $25 (Offline)
  • 2 d
 • Timothy & Michelle Wright 
  • $200 (Offline)
  • 8 d
 • tev monnin 
  • $100 
  • 9 d
 • Fatima A. Yasin 
  • $25 
  • 9 d
See all

Organizer and beneficiary

Tanzanian Diaspora in USA 
Organizer
Minneapolis, MN
Frank Minja 
Beneficiary
 • #1 fundraising platform

  People have raised more money on GoFundMe than anywhere else. Learn more

 • GoFundMe Guarantee

  In the rare case that something isn’t right, we will refund your donation. Learn more

 • Expert advice, 24/7

  Contact us with your questions and we’ll answer, day or night. Learn more